Popis: |
Kasi ya vijana katika kukuza muziki wa kizazi kipya katika kipindi cha utandawazi haiendani na kasi ya ukuzaji wa ngoma za asili. Mpaka sasa haujafanyika utafiti wa kina kuhusu kuzuka kwa tabia hii. Makala haya yanatumia mahojiano na vikundi vya ngoma vitatu halikadhalika wanamuziki wa kizazi kipya kuweka bayana chanzo cha tatizo. Aidha, makala haya yanatumia nadharia ya utendaji kama darubini kuchunguza matatizo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yanayowakumba vijana na namna yanavyochochea mfumuko wa tabia hii mpya. Utafiti huu umegundua kwamba uhaba wa mianya ya kiuchumi na kisiasa kwa vijana, nafasi ya ngoma za asili katika jamii ya sasa, mahusiano hasi kati ya vijana na wazee katika kuuendeleza utamaduni pamoja na vijana kutaka maendeleo ya haraka kuwa ndio chimbuko la tatizo. |