Popis: |
Katika makala hii ninalenga lugha mbili zinazoongewa na Wambugu wanaoishi Wilaya ya Lushoto katika milima ya Usambara ya nchi ya Tanzania. Mojawapo ya lugha hizo inaitwa Kimbugu cha ndani iliyo na miundo ya upatanisho wa ngeli na viiambishi awali wa kibantu huku ikiwa na nduni nyingi ambazo zinaonekana kutoka lugha kadhaa zisizo za Kibantu. Lugha hiyo Inafikiriwa kuwa aina moja ya lugha za mchanganyiko na inalengwa kama kadhia isiyo na kifani katika masomo ya migusano ya lugha. Lugha nyingine inayoitwa Kimbugu cha kawaida inafikiriwa kwamba inafanana sana na Kipare kinachoongewa na Wapare wanaoishi katika milima ya Pare. Lakini hakuna data za kina. Katika makala nyingine zilizoandika kuhusu lugha hizi zinatolewa taarifa kwamba lugha hizi zote ni lugha za Wambugu wenyewe na zinarithiwa kama lugha ya kwanza. Hata hivyo, hali ya matumizi ya lugha ambazo Wambugu wanaongea hazielezwi kwa kina hata mara moja. Kutoka uhakiki wa usuli wa uchaguzi wa Kimbugu cha ndani na cha kawaida kama huo, katika makala hii ninachanganua matumizi ya lugha ya Wambugu pamoja na matokeo ya utafiti niliofanya katika Wilaya ya Lushoto na ninahitimisha kwamba Kimbugu cha ndani na cha kawaida zinarithiwa kama lugha ya kwanza na makundi mawili tofauti, sio na kundi moja. |