'Gari ni Testing': Uhalalishaji wa Mahusiano ya Kingono Miongoni mwa Wazulufu Nchini Kenya

Autor: Catherine Wawasi Kitetu, Jonathan Furaha Chai, Raphael Mwaura Gacheiya
Rok vydání: 2022
Zdroj: East African Journal of Swahili Studies. 5:388-398
ISSN: 2707-3475
2707-3467
DOI: 10.37284/jammk.5.1.878
Popis: “My friend always tells me of how good it is... how sweet it is... when will I know these things?” Ulimwenguni, tafiti kuhusu tabia za wazulufu zimebainisha kuwa wazulufu hushiriki ngono za mapema licha ya ujamianaji kabla ya ndoa kukashifiwa. Imegunduliwa kuwa utamaduni, matumizi ya lugha na miktadha ya kijamii huwa na nafasi muhimu katika kuelewa na kuthibiti mahusiano na ushiriki wa ngono. Hata hivyo, ni kweli kuwa kutokana na mabadiliko ya jamii kiuchumi, kisiasa na kijamii, tamaduni hizi zimeasiwa na kupelekea itikadi ya kujihini na ubikira kutozingatiwa na wazulufu. Makala haya yanalenga kuangazia jinsi wazulufu kwa kuegemea peo za kimazungumzo wanavyohalalisha ngono za mapema miongoni mwao. Hili litaafikiwa kupitia Nadharia ya Uchanganuzi wa Peo kama ilivyoasisiwa na E. Goffman mwaka wa 1974. Data inatokana na mazungumzo katika vikundi kiini miongoni mwa wazulufu katika shule za upili nchini Kenya. Kwa kutumia nadharia ya uchanganuzi peo, inabainika kuwa wazulufu huhalalisha tabia za kujamiana na ngono za kabla ya ndoa kupitia peo nne za mazungumzo: upeo wa udharura, upeo wa kujihini, upeo wa mamlaka na upeo wa uanishi na utambulisho. Peo hizi za mazungumzo zaweza kuwa kiingilio muhimu cha kuwaelewa wazulufu na kuunda mbinu na sera mwafaka za kukabiliana na changamoto zinazowakumba
Databáze: OpenAIRE