Mitazamo ya Lugha na Utambulisho wa Kijamii Miongoni mwa Wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ
Autor: | Catherine Wawasi Kitetu, Raphael Mwaura Gacheiya, Peris Mwihaki Ndung’u |
---|---|
Rok vydání: | 2022 |
Zdroj: | East African Journal of Swahili Studies. 5:215-223 |
ISSN: | 2707-3475 2707-3467 |
DOI: | 10.37284/jammk.5.1.769 |
Popis: | Lugha ni kipengele muhimu cha utambulisho ambacho huweza kuwaunganisha, kuwatenganisha au kuwabagua wazungumzaji katika jamii. Utambulisho ni mtazamo wa kibinafsi wa mtu, yeye ni nani na vibainishi vinavyoashiria ushirika wake katika kikundi fulani cha kijamii. Mitazamo au maoni ya wazungumzaji kuhusu wao ni akina nani au utambulisho wao katika jamii, yanaweza kutofautiana na ushahidi wa kiisimu ambao huweka makundi ya wazungumzaji wanaozungumza lahaja mbalimbali kama wanajamii wa lugha moja. Dhana hii hudhihirika kwa wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ ambao huchukuliwa kuwa wao si Wakikuyu hata ingawa kiisimu wameainishwa na kuwekwa katika kundi moja kama Wakikuyu. Makala haya yanaazimia kuchunguza mitazamo wanayoendeleza wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ kuhusu utambulisho wao wa kijamii katika jamii. Mtazamo ni tathmini, chanya au hasi, kuelekea kitu au mtu, ambayo hujidhihirisha kwa imani, hisia au nia ya mtu mwenyewe. Kuna wakati wazungumzaji huweza kujinasibisha na kikundi fulani cha kijamii na wakati mwingine kukana utambulisho huo kutokana na sababu mbalimbali. Hii hutokana na wao kuendeleza mitazamo mbalimbali kuhusu utambulisho huo. Utafiti wa makala haya uliongozwa na nadharia ya Tajfel na Turner (1979). Data ilikusanywa kupitia mahojiano na kuchanganuliwa kimaelezo. Matokeo ya utafiti yalidhihirisha kuwa wazungumzaji wa Kĩndia na Kĩgĩchũgũ wana mitazamo hasi na chanya kuhusu utambulisho wao wa kijamii. Mitazamo hasi ya kubaguliwa na kudhalilishwa ilichangia watafitiwa kukana utambulisho wao na jamiilugha ya Wakikuyu na kujitambulisha kama Wakĩrĩnyaga. |
Databáze: | OpenAIRE |
Externí odkaz: |