Popis: |
Fujo, vita na uhasama uliibuka nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Huenda kuna sababu nyingi zilizochangia vurugu hizi, lakini inaaminika kwamba, mojawapo ya sababu hizi ni ukabila. Jambo moja linalodhihirisha makabila ni lugha. Makabila tofauti huongea lugha tofauti. Hata hivyo, tofauti za kikabila zinaweza kukabiliwa iwapo kutakuwa na lugha inayoeleweka kwa kila mtu. Lugha hii pia inafaa iwe ya kienyeji ndiyo watu waweze kujinasibisha nayo na kuielewa vyema (Thiong’o, 1992). Suluhu ni lugha ya Kiswahili. Lugha hii inaweza kuendeleza mbele nchi hasa katika kuleta umoja, uwiano na maendeleo. Makala haya yananuia kutambua jinsi tafsiri za Kiswahili za kazi mbalimbali zinavyoweza kuchangia katika maendeleo ya sekta mbalimbali na kuleta uhusiano mwema nchini Kenya. Pia, yatatoa mwangaza kwa serikali ya Kenya kuhusu mbinu mojawapo ya kuleta umoja, uwiano, amani na maendeleo kwa kuhusisha tafsiri za Kiswahili. |